UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan
MP3•Episode-Home
Manage episode 448479352 series 2027789
Inhalt bereitgestellt von UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Alle Podcast-Inhalte, einschließlich Episoden, Grafiken und Podcast-Beschreibungen, werden direkt von UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations oder seinem Podcast-Plattformpartner hochgeladen und bereitgestellt. Wenn Sie glauben, dass jemand Ihr urheberrechtlich geschütztes Werk ohne Ihre Erlaubnis nutzt, können Sie dem hier beschriebenen Verfahren folgen https://de.player.fm/legal.
Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani. Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka.OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi.Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo.Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka wakati mfumo wa huduma ya afya nchini Sudan umzidiwa uwezo, huku hospitali nyingi hazifanyi kazi au zimefungwa kabisa kutokana na usambazaji mdogo wa vifaa na uhaba wa mafuta. Shirika hilo linasema hadi asilimia 80 ya vituo vya afya katika maeneo yenye migogoro ikiwa ni pamoja na Al Jazirah, Kordofan, Darfur na Khartoum aidha havifanyi kazi au vimefungwa.Na linaonya kwamba "Kuporomoka huku kwa mfumo wa afya kunazuia mipango ya chanjo ya watoto, kuongeza kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayozuilika, na kuzua wasiwasi kuhusu uwezekano wa milipuko mikubwa zaidi ya magonjwa."Kwa sasa mashirika hayo yamesema majimbo yaliyoathirika zaidi na kipindupindu ni Kassala Gedaref, Al Jazirah, na Northern wakati homa ya kidingapopo imeghubika zaidi majimbo ya Kassala na Khartoum.Pia changamoto nyingine kubwa ya kutoa huduma za afya katikati ya milipuko hii mashirika hayo yanasema ni mashambulizi dhidi ya vituo vya afya ambayo tangu kuanza kwa vita 15 Aprili mwaka jana yamefikia 116 na kusababisha vifo 188 na majeruhi 140.
…
continue reading
100 Episoden