31 OKTOBA 2024
MP3•Episode-Home
Manage episode 447822512 series 2027789
Inhalt bereitgestellt von UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Alle Podcast-Inhalte, einschließlich Episoden, Grafiken und Podcast-Beschreibungen, werden direkt von UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations oder seinem Podcast-Plattformpartner hochgeladen und bereitgestellt. Wenn Sie glauben, dass jemand Ihr urheberrechtlich geschütztes Werk ohne Ihre Erlaubnis nutzt, können Sie dem hier beschriebenen Verfahren folgen https://de.player.fm/legal.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada kwa kina inayotupeleka Zanzibar nchini Tanzania kupata ufafanuzi wa jukumu la “Zanzibar Maisha Bora Foundation” akitueleza Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno HEREREZA.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na mashirika yake lile la mpango wa chakula (WFP) na la chakula na kilimo (FAO), uhaba mkubwa wa chakula unatarajiwa kuongezeka kwa ukubwa na ukali katika nchi na maeneo 22 duniani. Ripoti hiyo inaonya kwamba kuenea kwa migogoro, hasa katika Mashariki ya Kati inasukuma mamilioni ya watu ukingoni.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio la jana usiku lililotekelezwa na Jeshi la Urusi ambapo jengo la makazi la ghorofa nyingi lilipigwa katika mji wa Kharkiv, wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya majiji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewapigia chepuo vijana akitaka sauti zao na mawazo yao kupewa nafasi kwani kuanzia harakati za chinichini hadi maabara za uvumbuzi, vijana wanasukuma hatua kabambe kukabiliana na tabianchi, wanaunga mkono ujumuishaji wa nishati mbadala, kazi zisizozalisha hewa chafuzi na usafiri safi wa umma, ambayo ni mambo yanayochangia kuunda miji endelevu ambapo kila mtu anaweza kustawi.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEREREZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
…
continue reading
100 Episoden